Website counter

Home Picha Habari Siasa Michezo na Burdani Niandike Email: sugumalaria@gmail.com  

AMANI NA UTULIVU NDIO MSINGI WA MAENDELEO

 

 

 

 

 

 

 

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA
Magazeti Yetu
Kutoka Mitandao Mengine
Vyuo Vikuu
 
 
 
 
 
 

 

 

 

 

thread Jf

DK Slaa hacheki, hatabasamu?

Malaria sugu

sijawahi kumuona Dk slaa akitabasamu akiwa bungeni au hata kwenye vyombo vya habari.
jee ikiwa kiongozi wa nchi kama rais hata hutabasamu inaonyesha ni wazi hata wananchi wako watashindwa kucheka, watakuogpa na baya wanaweza kukona dikteta hasa ukiwa uanongoza watu wenye mila tofauti za kikoo.
lkn kweli dk slaa hacheki na hatabasamu?

Mh Dk Slaa

Wana JF,
Nadhani rafiki yangu Malaria Sugu ni mchokozi tu! Unacheka kunapokuwa na kuchekesha. Nadhani waliomjib ni sahihi. Sina hakika kama Malaria Sugu anafuatilia matukio yote, tangu nilipotamka ndani ya Bunge kuwa ..."Nchi inateketea" kwa ufisadi. Nikapigwa stop na Wabunge, Mawaziri, na hata Spika akataka nifute kauli ya nchi kuteketea. Kama Bunge linashindwa kutambua nchi inateketea kwa mabilioni yaliyoibiwa, bado unacheka basi utakuwa mwendawazimu. Nilikataa kuwa mwendawazimu, ndio maana nikaenda na wenzangu MwembeYanga kutangaza majina ya wanaoiteketeza Taifa, baada ya kuona Bungeni hakuna matumaini, japo baadaye, wengi wa hao walionipiga stop wamepiga U turn kubwa angalau kwa maneno. Lakini kusema kweli kipindi hiki si cha kutafuta kicheko na Tabasamu, ni cha kuomboleza tukiona nchi inaendelea kuangamia na sitegemei mtu anayeipenda nchi yake atakuwa katika hali ya kutabasamu, isipokuwa kama ni tabasamu ya kinafiki. Namwomba radhi kama nitakuwa nimemwudhi MalariSugu. Nimezoea kuwa mkweli, na ninaumia moyo, hivyo siwezi kuvaa unafiki wa kucheka eti kwa sababu wananchi wataogopa. Ni vema waogope kama hilo litasaidia kuokoa Taifa na rasilimali zake.

 

 

Re: Dr. Slaa kapotelea wapi?

Malaria sugu

SHKAMOO DK SLAA. KATIBU MKUU NA ALIEKUWA MGOMBEA URAIS WA CDM.
Swali no 2.
I)Ubunge ulianza lini. jee kwanini wakati wa mkapa wakatu ulikuwa mbunge ulikuwa kimya sana tofauti na sasa. jee hakuna harufu ya udini hapa?

Mh Dk Slaa

Malaria Sugu,

Ninalijibu swali kwa manufaa ya Watanzania wengine. Wewe umekuwepo jamvini na unajua majibu yangu. Ndiyo maana nimesema ni vema mkatambua "time is Money" kuuliza maswali yasiyo na tija na kupoteza muda wa watu wengine ni Ufisadi kwa kukuwa tunawapotezea muda wale wenye nia ya kuuliza maswali yenye tija na yenye nia ya kulikomboa Taifa letu ambalo kila kukicha linaendelea kuporomoka. Malara Sugu, rudi kwenye "Hansard", Hotuba iliyotoa nyaraka za awali za Anbem na TanpowerResources Ltd ni ya nani.

Nani aliyemwambia Mkapa alipe Kodi ya Pango kwa kufanya biashara kwenye Jengo letu Tukufu lano 15 Luthuli Street(Ikulu). Ushabiki bila kutumia kichwa haitatufikishamahali, na tumechoka kuzungukia hoja hizo hizo kama pia. We need to move forward, patience is giving up. Niliyoyaona Kisarawe yanatisha, na tusipokuwa makini "laana itaangukia kizazi hiki kwa kutochukua hatua". Ni vema weekends mka take time out kwenda vijiji ambavyo vinazunguka jiji la Dar. Tuki experience real life tutaacha kuzungumzia nadharia ambayo haina.

We need to discuss real issues about our country. Sina nia ya kuzuia watu kuzungumza kwani ni uhuru wao, lakini jikes na ushabiki ni vema yakaenda kwenye threads zinazohusika. Tunapunguza hadhi ya JamiiForums. Lets all have sense of urgency to seek for appropriate solutions.

 

 

 

 

Copyright © 2011 Malaria Sugu. All rights reserved.